URUSI YAKANA KUISHAMBULIA KIMTANDAO UJERUMANI


KWA UFUPI: Mifumo ya kimtandao katika baadhi ya wizara za serikali ya Ujerumani ilikumbwa na udukuzi uliopelekea kuibiwa kwa taarifa kadhaa huku baadhi ya vyombo vya habari vimeishutumu Urusi dhidi ya shambulizi hilo la kimtandao. Nae waziri wa Ujerumani wa maswala ya uchumi akieleza hawana uhakika kua Urusi imehusika na shambulizi hilo. Aidha, Urusi  imekana kuhusika na shambulizi hilo.

——————————————


Mataifa makubwa yenye uwezo wa kimtandao yamekua yakishutumiana panapo tokea mashambulizi mtandao kwenye mataifa hayo. Urusi, Uchina na Korea ya Kaskazini wamekua wakishtumiwa Zaidi na mataifa ya Ulaya na marekani.


———————

TAARIFA: Tume ya TEHAMA ya nchini Tanzania imekaa kikao chake cha kwanza mahsusi kujadili maswala ya usalama mtandao Nchini ambapo mengi yalipata kuangaziwa na lengo kuu limekua ni kuhakiki tunapata taifa salama kimtandao.

———————


Ujerumani Hivi karibuni imekumbwa na shambulizi mtandao katika wizara zake mbili hadi sasa ambao umepelekea taarifa kadhaa za wizara hizo kupotelea mikononi mwa wahalifu mtandao.


Wabunge wa Ujerumani wametupia lawama serikali kwa kutokuwaambia kuhusu mashambulizi hayo ya mtandaoni huku kamati ya masuala ya dijitali ya bunge la Ujerumani ikiketi kwa dharura kwa madhumuni ya kuipitia taarifa juu ya udukuzi huo ulio gundulika Mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu wa 2018.

Mmoja wa wajumbe wa kamati ya digitali – Anke Domscheit-Berg, kutokea chama cha mrengo wa kushoto, Die Linke ame eleza ya kua serikali ya ujerumani ilipaswa kujua mashambulizi hayo ya kimtandao mapema na kuyadhibiti.Shirika la habari la Ujerumani, DPA, lilivinukuu vyanzo vya usalama ambavyo havikutajwa majina vikisema kwamba kundi la APT28 la Urusi lilidukuwa mifumo ya mawasiliano ya wizara za mambo ya nje na ndani za Ujerumani na kufanikiwa kuiba taarifa.


Shirika hilo linasema kuwa mashambulizi hayo yaligunduliwa mwezi Disemba mwaka jana na inawezekana yalikuwa yakiendelea kwa mwaka mzima.


Thomas de Maiziere.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani
Kufuatia ripoti hiyo, wizara ya mambo ya ndani ilithibitisha kudukuliwa kwa kompyuta za serikali kuu ya shirikisho, ikisema kuwa mashambulizi hayo yalifanyika kwenye masuala yasiyohusiana na siri za serikali na kwamba yalidhibitiwa.


Hata hivyo, msemaji wa wizara hiyo hakuweza kutoa undani zaidi wa suala hili, akisema limo kwenye uchunguzi na kwamba hatua za kiusalama zinaendelea kuchukuliwa.


Lakini kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Ujerumani, udukuzi uliachiwa kuendelea hadi Februari 28 ya mwaka huu wa 2018 ili wachunguzi wakusanye taarifa kuhusiana na upana, malengo na watendani wenyewe.


“Ikithibitika kuwa ni kweli, hivi vitakuwa ni aina ya vita dhidi ya Ujerumani,” alisema mkuu wa kamati ya masuala ya dijitali ya bunge la Ujerumani, Dieter Janacek, kutoka chama cha walinzi wa mazigira, Die Grüne, kwa mujibu wa gazeti la Berliner Zeitung.

Janacek aliyataja mashambulizi hayo kubwa ni mabaya kabisa, na ametoa wito kwa serikali kuzifikisha taarifa zote ilizonazo bungeni.


Vikao vya kwanza vya Usalama Mtandao vilivyo andaliwa na Tume ya TEHAMA Nchini Tanzania 
Alipoulizwa endapo mashambulizi hayo yalifanywa na kundi linaloungwa mkono na Urusi, mbunge kutokea muungano wa CDU/CSU wa Kansela Angela Merkel, aliutetea mkakati wa serikali kuzuia taarifa. Stephan Mayer kutoka chama cha CSU alisema “uchunguzi kamili na wa kina” ulikuwa unahitajika “lakini sio wa kuwekwa hadharani.” Mbunge huyo aliongeza kuwa “kuwadhania vibaya wengine hakuwezi kuusaidia uchunguzi huo”.


Kundi la APT28 au wakati mwengine huitwa Fancy Bear, ambalo linahusishwa na idara ya ujasusi kwenye jeshi la Urusi, limewahi kutajwa kuhusika na mashambulizi  ya mtandaoni dhidi ya Bunge la Ujerumani mwaka 2015 na pia ofisi za Jumuiya ya Kujihami ya NATO na serikali za mashariki mwa Ulaya.


Brigitte Zypries
Waziri wa Nishati na Uchumi
Ujerumani.
Tayari waziri wa nishati na uchumi wa Ujerumani Mh. Brigitte Zypries amezungumzia shambulizi hili na kueleza yakua hakuna Ushahidi unaothibitisha ya kua Urusi ndio imehusika.


Aidha, Urusi nayo imekana kuhusika na shambulizi hilo.

By admin